Wafanyakazi wa SUA kampasi ya Solomon Mahlangu waukaribisha mwaka mpya 2023

Siku ya ijumaa tarehe 3 Feb 2023, wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kampasi ya Solomon Mahlangu (SMC), iliyopo Mazimbu Morogoro, walikutana kwenye sherehe ya kuuaga mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka 2023.

Lengo la hafla hii ni kuleta watumishi  wa SMC pamoja kufurahi katika kula, kunywa na burudani zingine ili kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya. Sambamba na hilo, hafla hii hutumika kutambulisha waajiriwa wapya, waliohamia na wanaorudi toka masomoni.

Maongezi na vinywaji
Maongezi na vinywaji …
Mawili matatu toka kwa viongozi
Burudani safi kabisa…
Burudani murua toka kwa magwiji wa dance toka idara ya TEHAMA
Karibuni wote kupata chakula
Maongezi na chakula

 

 

Related Posts